
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuiagiza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufuatilia sakata la kupotea kwa Mwanafunzi huyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Joseph Kusaga amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji wale wote aliwataja kwenye ujumbe aliocha kabla ya kuondoka
Mkuu wa shule ya sekondari ya Pandahill Brother Zephania Lusanika amesema kuwa mwanafunzi huyo aliacha ujumbe altareni na kwamba moja ya sababu zilizofanya washindwe kuelewa namna alivyo ondoka ni kutokana na kamera CCTV kuzimwa kupisha zoezi la mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka huu