Jumamosi , 14th Jun , 2025

Klabu ya AS Monaco ipo katika mazungumzo na  mchezaji wa zamani wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba kwaajili ya kusamjili  kwa mkataba wa miaka miwili.

Paul Pogba

Paul Pogba mwenye umri wa miaka 32 amewahi kucheza  kwa mafanikio makubwa akiwa na Juventus ya Italia akiisaidia Kibibi Kizee cha Turin  kuchukua kombe la Serie A mara nne, Super cup mara tatu pamoja na Coppa Italia mara tatu. 

Kiungo huyo aliyeshinda kombe la Dunia 2018 akiwa na timu yake ya  taifa ya Ufaransa anatarajiwa kurejea katika ardhi yake ya nyumbani baada ya kuanza mazoezi wiki kadhaa zilizopita kabla ya kuanza kipindi cha pre season

Pogba alikuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima baada ya kufungiwa kutokana na kukutwa na hatia ya kutumia dawa zilizozuiliwa michezoni .