Taarifa ya TPLB imeeleza kuwa ligi hiyo inataraji kumalizika mnamo Mei 24-2025 huku ikihusisha mizunguko 30 huku dirisha dogo la Usajili likitaraji kufunguliwa Desemba 15 mpaka Januari 15-2025
Bingwa Mtetezi wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita 2023-24 ni klabu ya Yanga SC huku timu mbili ambazo zimepanda kwa msimu huu ni pamoja na timu za Kengold FC kutoka Tukuyu Mbeya na Pamba Jiji FC kutoka Mwanza
Upande mwingine,Ligi daraja la Kwanza maarufu kama Championship yenyewe inataraji kuanza mnamo Septemba 14-2024 huku ikitaraji kumalizika mnamo Mei 10-2025 huku mchezo wa fainali ya kombe la FA utachezwa mnamo Mei 31-2025