Jumatano , 7th Jun , 2023

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya katiba na sheria zimesaini mkataba na serikali ya ujerumani kupitia shirika lake la maendeleo GIZ wenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 12.6 kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wanawake na watoto.

Mkataba huo wa miaka mitatu umeingia hii leo ukilenga kuwajengea uwezo taasisi zinazotoa msaada wa kisheria,kuwajengea uwezo wanawake na watoto ili kupunguza ukatili wa kijinsia katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa niaba ya waziri wa katiba na sheria mkataba hup umetiwa saini na Katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt Mary Makondo.

Aidha Dkt Mary amesema utekelezaji wake unakwenda sambamba na kampeni ya wizara kuhusu msaada wa kisheria ya Iliyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo changamoto za mirathi,mali mashambulio kwa wanawake na watoto yanazingatiwa.

Kwa upande wake balozi wa Ujerumani nchni Tanzani Regine Hess amesema suala la ukatili wa kijinsia ni sio tu la Tanzania peke yake ni janga la kidunia halina budi kuchukiwa na walinda haki za binadamu na kwamba wao kama Ujerumani wako tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya unyanyasaji kwa Watoto na wanawake.

Imesisitizwa kuwa suala la changamoto za mila na desturi bado ni changamoto pia kwa baadhi ya elimu hivyo mkataba huo unakwenda kuongeza elimu na msaada wa Kisheria.