
Picha ya Mbosso upande wa kushoto, kati Mkubwa Fella na kulia ni Enock Bella
Enock ameomba msamaha huo baada ya Mbosso kuzungumza na waandishi wa habari kusema anasononeshwa na Enock anavyomzungumzia kwa watu.
"Sisi ni ndugu Mbosso wengi watahitaji kulitumia hili jambo kama fursa maana haya yote yalishapita. Nisamehe kwa kila nilipokukosea nakumbuka nilishawahi kukwambia before neno hili"
"Muziki uendelee undugu wetu hauwezi vunjika bro Room Number 3 ndio habari ya mjini" - Ameandika Enock
Wawili hao wamewahi kuwa chini ya kundi la Yamoto Band ambalo lilifanya vizuri kwenye muziki wa BongoFlava.