
Mwanafunzi aliyejinyonga
Taarifa za kifo cha Emmaus zimethibitishwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, ingawa sababu za kifo chake bado hazijafahamika.
Akizungumza Boniface Zackharia ambaye ni rafiki wa marehemu amesema kuwa," Ni kweli majira ya saa 5:00 asubuhi leo Juni 22, 2025, alikutwa bafuni anakokaa amejinyonga, chanzo hakijajulikana kwa sababu asubuhi tumeamka tulikuwa sawa kabisa, na asubuhi nilimuacha anasubiri maji yajae kwenye ndoo ili akaoge nimefika kwenye majukumu yangu dakika chache sana nikapigiwa simu na jirani mwingine kwamba Emmaus kajinyonga sikuamini,".
Aidha rafiki huyo ameongeza kuwa, "Wakati familia inaendelea na taratibu zingine nadhani mwili utaagwa Jumanne na utasafirishwa moja kwa moja kwenda nyumbani Bukoba mkoani Kagera,".