Ijumaa , 27th Jun , 2025

Baada ya klabu ya  Mamelodi Sundowns FC kutoa sare hapo jana dhidi ya klabu ya Fluminense kutoka Brazil, imewafanya  kuwa  moja ya timu kutoka Africa kutolewa  katika michuano hii.

 

Mamelod wamemaliza wakiwa  nafasi ya tatu wakiwa wamekusanya alama nne, alama ambazo wamezipata baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya klabu ya  Ulsan HD FC kutoka Korea kusini huku akitoa sare dhidi ya klabu ya Fluminense na kufungwa dhidi ya Borussia Dortmund, hata hivyo hii ndiyo timu  kutoka barani Africa iliyokusanya alama nyingi zaidi wakiwa wamekusanya  alama nne.

Inafuatiwa na klabu ya Esperance ya Tunisia ambayo imekusanya alama tatu hii ni baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya klabu ya Los Angeles FC kutoka Marekani huku wakipoteza dhidi ya Chelsea na Flamengo kutoka Brazil.

Klabu ya mwisho ni klabu ya Wydad Casablanca ambayo mpaka sasa imecheza michezo miwili dhidi ya Juventus na Manchester city na kupoteza michezo yote. 

Leo Wydad Casablanca wanakamilisha ratiba dhidi ya Al-Ain kutoka United Arab Emirates, Jambo linalosubiriwa kwa hamu ni kuona kama  Wydad Casablanca watafanikiwa kukusanya walau alama moja katika michuano hii.