Ijumaa , 27th Jun , 2025

Mahakama Kuu Masijala Ndogo Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, Julai 11, 2025.

Mahakama Kuu Masijala Ndogo Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, Julai 11, 2025.

Lissu amefungua shauri la maombi mahakamani hapo akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni, ulioyolewa Juni 2, 2025.

Hata hivyo, Serikali imeweka pingamizi hoja hiyo ikiiomba mahakama itupilie mbali maombi yake ikiwasilisha sababu sita.

Katika sababu hizo Seriali imedai kuwa maombi hayo yanakiuka kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinachozuia rufaa au mapitio dhidi ya uamuzi au amri ya mahakama isiyomaliza shauri la msingi.

Pia Serikali inadai mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kulingana na moja ya mambo anayoyaomba ambayo yanalenga kuifanya mahakama iangalie kama kifungu cha 188 cha sheria hiyo kinakiuka ama hakikiuki Katiba.