
Vizimba soko la Magomeni
Wafanyabiashara katika sehemu za juu za jengo la soko la Magomeni waliteremka chini na kufanya biashara huko kwa kile kilichodaiwa kuwa wateja hawafiki juu ghorofani. Badhi ya wafanyabiashara hao wamedai kuwa hata sasa bado hali sokoni hapo siyo nzuri kibiashara.
Wenyeji katika soko hilo wanasema kulikuwa na tabia ya mazoea ambayo wafanyabiashara walijijengea kwamba hauwezi kupata wateja kama upo juu na kwamba ndiyo imekuwa ikiwasumbua wafanyabiashara sokoni hapo. Alex Kobela ni mfanyabiashara sokoni hapo ambaye EA radio imefanikiwa kuzungumza nae juu ya hali ya biashara sokoni hapo.
“Kulikuwa na tabia ya mazoea ambayo wafanyabiashara walijijengea kwamba hauwezi kupata wateja kama upo juu na hii ndiyo imekuwa ikiwasumbua wafanyabiashara hapa. Hili soko limejengwa kwa viwango vya kimataifa na wafanyabiashara lazima wake kwenye maeneo yaliyopangwa kutegemea na anachokiuza. Kwahiyo pale chini walikuwa wanavunja utaratibu, hata hivyo Tunashukuru sasa hivi tumefanikiwa kuwarejesha tena kwenye maeneo wanayostahili kulingana na anachokiuza ili soko liwe na mpangilio.”- Formela Kanyika, Mhasibu wa Manispaa ya Kinondoni.