
Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri Mulamula ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wafanyanyabisha kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba “Bukoba Expo" yaliyofanyika katika Viwanja ya CCM mjini Bukoba. Maonesho hayo yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “Biashara, viwanda na utalii ni fursa ya uwekezaji Mkoani Kagera”.
Mtakumbuka kuwa Tanzania pamoja na kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia ni mwanachama wa SADC na hivi karibuni tumeridhia mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (Africa Continental Free Trade Area-AfCFTA).
Eneo Huru la Biashara la Afrika ni soko kubwa kuliko masoko yote yaliyoanzishwa ulimwenguni kwa kuwa na uwingi wa nchi wanachama zinazofikia 55. Soko hili linakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao Bilioni 1.3 na Pato ghafi la Taifa (GDP) lenye jumla ya Dola za Marekani trilioni 3.4 na fursa za uchumi unaokua kwa kasi. Alieza Waziri Mulamula
Akizungumzia kuhusu maonesho hayo Waziri Mulamula ameleeza kuwa ubunifu wa waandaji umeakisi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Mkoa wa Kagera na wananchi wake wanapata maendeleo kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi, biashara na uwekezaji kwa kutumia fursa zilizopo katika Mkoa huo na nafasi ya Kijiografia ya Mkoa kwa kupakana na nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.