Jumanne , 5th Aug , 2025

Alphonce Temba, aliyekuwa akigombea kupitishwa kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema mojawapo ya mipango yake mikuu ilikuwa ni kuhakikisha mabasi yote ya mikoani yanarejeshwa kwenye Stendi ya Magufuli - Mbezi.

 

 

Akizungumza baada ya safari yake ya kisiasa kukwama kwenye mchujo wa wajumbe, Temba alisema lengo la mpango huo lilikuwa ni kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam, huku pia akilenga kuboresha huduma za usafiri kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali.

 

“Niliwaambia wajumbe nikipata Jimbo la Kibamba mabasi yote yaliyopo nje ya stendi ya Magufuli yatarudi pale iwe kwa kutungwa sheria Bungeni au la!'' alisema Temba.

 

Ameongeza kuwa ingawa nafasi ya kupeperusha bendera haikupatikana mwaka huu, nia yake ya kuleta mabadiliko bado ipo palepale, na anaendelea kutafakari njia nyingine za kuwatumikia wananchi wa Kibamba na Tanzania kwa ujumla.