Jumatatu , 4th Aug , 2025

Dar es Salaam: Mchambuzi wa masuala ya siasa, Godfrey Mchungu, amesema kuwa kati ya vyama sita vya ukombozi vilivyobaki barani Afrika, ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee kinachobeba hadhi na nafasi ya kuwa chama kiongozi katika kundi hilo.

 

Akieleza kwa kina, mchambuzi huyo alivitaja vyama hivyo kuwa ni ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe), pamoja na CCM kutoka Tanzania.

“Kwa msingi wa historia, chimbuko la mshikamano wa vyama hivi na harakati nyingi za ukombozi barani Afrika vilianzia Dar es Salaam,” alisema.

Ameongeza kuwa Tanzania kupitia CCM, si tu kwamba ilitoa hifadhi kwa wapigania uhuru, bali pia iliweka mazingira ya kisiasa na kiitikadi yaliyochangia uundwaji wa umoja wa vyama hivyo jambo linaloifanya ibaki kuwa nchi yenye ushawishi mkubwa kwenye siasa za bara la Afrika.