
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Biashara ya jumuiya hiyo (EABC), Bw.John Bosco Kalisa.
Lengo la ziara hiyo ni ni kuvumbua nafasi za kibiashara zinazopatikana nchini Congo
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Biashara ya jumuiya hiyo (EABC), Bw.John Bosco Kalisa, amesema kuwa mara baada ya Rais wa Congo Félix Tshisekedi kutia saini hati ya makubaliano ya kujiunga na jumuiya hiyo, mpango uliopo ni kukuza biashara baina ya nchi hizo
Wanapanga kusafiri wiki ya kwanza ya mwezi May na wanatamani sana kuwaona wafanyabiashara kutoka Congo, amesema Kalisa na kuongeza kuwa
Kila upande upo tayari kwa ziara hiyo, na mpaka sasa tayari tumeshaanzisha mwingiliano mzuri na shirikisho la wafanyabiashara wa Congo, wamekubali , amesema Bw. Kalisa akielezea pia mbali na kutembelea mji mkuu wa Kinshasa, pia viongozi hao watatembelea majiji ya mashariki mwa nchi ya Goma na Bukavu.
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Peter Mathuki, amesema kwamba vijana wanaweza kutazama fursa kwa wakati katika ukanda huu ambao sasa una wanachama 7 wa jumuiya
Nchi ya Congo inaongoza duniani kwa uzalishaji wa madini ya cobalt, ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa betri za kuchaji kwa ajili ya magari ya umeme na pia ni malishaji mkuu wa madini ya kopa.