
Matikiti
Wakizungumza na EATV wafanyabiashara wa matunda na nafaka za chakula akiwemo Tano Kiando, leo Aprili 14, 2022, wamesema kwamba kwa sasa kuna uhaba mkubwa wa matunda sokoni hapo pamoja na uhaba wa nafaka kama vile mahindi.
"Kiukweli mahindi yameadimika ni kwasababu ya kupanda kwa bei ya mbolea kule shambani, mbolea imepanda mno, kwahiyo tunanunua mahindi kwa bei ya juu sana kwa sababu gharama za uzalishaji zimepanda, kingine ni kupanda kwa bei ya mafuta, tunajikuta tunatumia gharama kubwa sana kusafirisha mahindi, tunatumia hadi milioni 1.6 kukodi fuso, tofauti na mwaka jana," amesema Tano Kiando
Kwa upande wake mwenyekiti wa soko hilo Francis Mulamula, ambaye pia ni mfanyabiashara wa mapapai amebainisha sababu ya matunda kuadimika sokoni hapo.
"Kama mnavyoona upatikanaji wa matunda na nafaka katika soko hili umekuwa mgumu sana, matunda kama maembe, machungwa hayapo kabisa, hali hii inasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta, hali ya uchumi ni ngumu," amesema Francis