Jumatatu , 12th Jan , 2015

Wachimbaji haramu wa madini kutoka mikoa mbalimbali nchini wamevamia na kuharibu vyanzo vya mradi mkubwa wa maji unaotarajiwa kujengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bil 6 wilayani Muheza.

Chanzo cha Mradi mkubwa wa maji Muheza

Wachimbaji haramu wa madini kutoka mikoa mbalimbali nchini wamevamia na kuharibu vyanzo vya mradi mkubwa wa maji unaotarajiwa kujengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bil 6 kiwango ambacho kimeahidiwa kutolewa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia 88% ya wakazi wa wilaya ya Muheza kukosa maji.

Eatv imeshuhudia uharibifu huo mkubwa unaoendelea kufanywa katika chanzo kikuu cha maji yanayotegemewa na wakazi wa jiji la Tanga na Muheza kufuatia kamati ya ulinzi na usalama chini ya mwenyekiti wake wilayani Muheza Subira Mgalu ambaye amekemea vikali kuwa serikali haitavumilia kuona uharibifu huo ukiendelea hata kama sheria zimekinzana kwa sababu asilimia 88% ya wakazi wa Muheza hawana maji.

Mbali na uchimbaji madini pia baadhi ya wakazi wa vijiji mbalimbali,w afanyabiashara kutoka mikoa tofauti nchini kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji wameharibu vyanzo kwa kuvamia msitu wa hifadhi wa Usambara Mashariki na kuvuna miti kisha kupasua mbao ambazo inadaiwa kuwa huzisafirisha ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo inazifanya kamati za maizingira zinapofanya doria hasa nyakati usiku hutishiwa maisha na makundi hayo.

Kufuatia hatua hiyo kaimu afisa misitu wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Jackson Saria amekiri kuwepo kwa hujuma hizo lakini amelalamikia watendaji na wananchi kushindwa kuwapatia taarifa hizo na badala yake wanakwenda moja kwa moja kwa mhifadhi mkuu wa msitu wa Usambara mashariki na kwa mkuu wa wilaya ya Muheza.