Ijumaa , 5th Dec , 2014

Kama sehemu ya utetezi wa kubadilika sana kwa muziki wake, Rapa Stereo amesema kuwa, mashabiki pia ama wasikilizaji wa muziki wa Hip Hop nao wamegawanyika huku wakiwa na mapenzi ya kusikiliza aina fulani ya hip hop.

Msanii wa miondoko ya hip hop nchini, Stereo

Aina hiyo ya hip hop ambayo yapo ni kuanzia katika siasa, mapenzi, majigambo binafsi, hatua ambayo humfanya msanii kujiwasilisha katika ladha tofauti tofauti.

Stereo akitolea mfano ujio wa kazi yake mpya 'Ukonga Mikono Juu', amesema kuwa baada ya kugusa sehemu tofauti za muziki huu, ameamua kusikiliza maoni ya mashabiki wengi na kurudi tena katika Hip Hop ya mtaa, akionesha mfano kwa kuwakilisha vizuri sehemu anayotoka, katika kazi hiyo.