Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia amaesema;
"Tumefuta VAT ya nyasi bandia ili kuboresha viwanja vya michezo, na hapa nizungumze na chama changu cha Mapinduzi, viwanja vingi hivi vinamilikiwa chama cha Mapinduzi lakini hali yake hairidhishi sasa fursa imetoka niombe sana viwanja vitengenezwe viwekwe nyasi bandia ili vijana wetu watumie viwanja hivyo na wajiendeleze kimichezo lakini walipe thamani ya ile pesa wanayoitoa kutumia viwanja hivyo"
"Hivyo basi namtaka Naibu katibu mkuu ambaye yuko hapa kuandaa program ya kuviboresha viwanja hivyo na kama hamna uwezo tafuteni wawekezaji muingie nao kurekebishe kazi hiyo".