Mfano wa mwanafunzi mjamzito (Picha kutoka mtandaoni)
Wakizungumza na EATV kijijini hapo,Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, wananchi hao wamesema watoto wao wanapata ujauzito kutokana na kutembea umbali wa kilometa 30, kwenda na kurudi shuleni hali iliyowalazimu wananchi wa kijiji hicho kujitolea kujenga shule karibu ili kunusuru hali hiyo.
“Kwakweli hapa Matale tunashida wanafunzi wetu tunawapeleka shule nyangoroka , somanga kule hawamalizi shule wengi wanaishia njiani, wavulana hawamalizi shule sababu ya umbali wasichana wengi wamepata mimba sisi wananchi tumeanzisha ujenzi wa sekondari ila bado tunaomba watusaidie tumalize haya madarasa wanafunzi wetu wapate pakujisomea” amesema Mwasi Ozananke mkazi kijiji cha Mtale .
Aidha licha ya jitihada walizofanya kuwakomboa watoto hao badoa wameiomba serikali pamoja na mbunge wao kuwasaidia iliwaweze kukamilisha ujenzi huo kuwanusuru watoto wao kwani hawajabahatika kupata sekondari huku wakieleza hali halisi kijijini hapo kuwa wakifaulu watoto 60 kwenda sekondari wanaomaliza ni wane tu.
Zaidi ya wanafunzi 54 wa Shule ya Sekondari kutoka Kijiji cha Matale, Wilaya ya Bariadi, wamekatisha masomo yao kutokana na kubeba ujauzito.