
Queen Suzy
Akiongea na eNewz ya East Africa TV, Suzy amesema kuwa kinachompa mafanikio siyo pesa za wanaume bali juhudi alizozionesha mpaka kupata tuzo.
“Nimepewa tuzo kwa sababu ya unenguaji siyo kuhongwa wala kudanga, jasho langu katika kazi ndiyo limenibeba. Hakuna wakunishinda kiuno kimenipandisha ndege na kunipa nyumba nimejenga mbezi na nina viwanja”, amesema Suzy.
Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuwaruhusu watoto wao kuonesha vipaji vyao. "Nawaomba wazazi waruhusu watoto wao wenye vipaji kuonesha walichonacho, siyo matusi ni kiuno ndiyo kimenipa umaarufu nchini".
"Tanzania nzima mimi ndiye Rais wa wanenguaji sina mpinzani, mimi ni raisi wa milele. Napewa mshahara situmii kiki najituma“, ameongeza.