Alhamisi , 30th Oct , 2014

Mashindano Ngumi ya Taifa yanatarajiwa kufanyika Desemba 3 mpaka 9 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha vyama vya mikoa na vilabu mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Nchini BFT, Lukelo Willilo amesema mashindano hayo yanalenga kutafuta timu ya taifa ya vijana ambayo itakaa kambi ya muda mrefu kwa ajili ya kujiandaa kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Lukelo amesema kutokana na mashindano hayo kuwa ya wazi, wamepanga kufanyia katika eneo ambalo wanaamini mashabiki wa mchezo huo wataweza kufika kwa wingi ambapo eneo hilo ni Tanganyika Parkers au viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es salaam.