Wafanyabiashara nchini wameaswa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na badala yake wametakiwa wasimamie utekelezaji wa masharti ya leseni zao kwa mujibu wa sheria, taratibu pamoja na kanuni za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na mmoja ya wafanyabiashara nchini ambao huusika na ukusanyaji wa madeni ya serikali bi Scolastica Kevela ambaye amewataka wafanyabiashara kutojihusisha na vitendo Hivyo kwa kuwa uzoefu uunaonesha wapo Watu wasiowaaminifu hukitumia kipindi hiki Cha Uchaguzi Mkuu kukiuka misingi ya kibiashara.
Aidha amesisitiza kuwa kwa Sasa ni vyema kutumia fursa zitakazotokana na uchaguzi huku akiwaasa wafanyabiashara wengine kuzidi kufanya uwekezaji bila hofu kwa kuwa Tanzania kihistoria imekuwa ikipita katika chaguzi zake bila Uvunjifu wa Amani.
Akihitimisha amewataka pia wananchi kuendelea kusimama imara ili kwa Pamoja kukua kiuchumi zaidi ya Uchumi wa Kati ambao Kama nchi imefikia kwa sasa "Uwekezaji uliopo bado una changamoto licha ya kuwa atakayestahimili katika biashara ni yule pekee mwenye msingi imara na anayezingatia kanuni za uwekezaji" alisema Kevela