Msanii Msami Baby
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Msami Baby amesema hana matumizi makubwa na hatembeagi na pesa mfukoni mara nyingi huwa anatumia kadi au kufanya miamala kutumia njia ya simu.
"Mimi sio mtu wa kutembea na Cash napenda kutumia kadi na miamala mingine kwenye simu, kwa hiyo kilichokuwepo kwenye akaunti yangu ndicho naweza kufanya matumizi au ku-deal nacho, na kwenye matumizi inategemea naenda wapi, kwa tukio gani au mazingira ambayo nipo" amesema Msami Baby.
"Napenda kuishi kwa bajeti halafu mimi ni mbahili sana, pesa yangu haitumiki hovyo situmi na yakutolea, ukiniambia nitume kiasi nitatuma hichohicho ambacho tumekubaliana kama utataka ya kutolea itabidi uweke kwenye maongezi yetu kabla, ila mambo ya kujiongeza na kutolea huwa sina". ameongeza