Jumatatu , 11th Mei , 2020

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, amekanusha taarifa za kwamba yeye ni mgonjwa na hali yake ni mbaya, zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile.

Dkt Ndugulile amezikanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Mei 11, 2020, na kusema kuwa taarifa hizo zipuuzwe kwamba yeye ni mzima wa afya.

"Tupuuze taarifa za uzushi zinazosambazwa kuhusu afya yangu, niko mzima kabisa na ninaendelea na majukumu yangu, pole nyingi kwa walioguswa na taarifa za uzushi" ameandika Waziri Ndugulile.