Jumatatu , 2nd Mei , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii iwekeze kwenye miradi ya Maendeleo ikiwemo viwanda ili kujipatia wananchama wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi zaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,

Akizungumza jana katika katika Sherehe za Siku ya Mfanyakazi duniani ambapo kitaifa ilifanyika Mkaoni Dodoma,rais Magufuli amesema uwekezaji wa kwenye viwanda unakua ni wa muda mrefu na uhakika wa kuwa na wanachama wengi wa kudumu.

Rais Magufuli ameongeza kuwa endapo mifuko hiyo itaendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa Madaraja au Makalvati, wafanyakazi wake wanakuwa ni wa muda mfupi mara baada ya kukamilika kwa mradi huo hakutakuwa na mikataba tena ya wafanyakazi hao.

Amesema kuwa mifuko mingi ya hifadhi ya jamii ilikua iaingia kwenye miradi ya ajabu ajabu isyokuwa na tija huku akitaka kuwekeza kwenye viwanda vya kutengenezea bidhaa kama ngozi au viatu ambapo vijana wengi watapata ajira na kujenga uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amechukua ushauri wa shirikisho la Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), wa kupunguza mifuko ya hifadhi ya jamii na kubaki miwili na kusema ushauri huo unafanyiwa kazi.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzia uwekezaji