
Mtangazaji T-Bway 360 na mpenzi wake Kim Nana
Akizungumzia kuhusu mahusiano yake na Kim Nana, kipindi cha ujauzito hadi kuwa mzazi kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio,inayoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 4:00 Asubuhi - 6:00 Mchana, TBway amesema,
"Kim Nana siyo Slay Queen, nilianza naye mahusiano muda mrefu sana kama miaka mitano au sita iliyopita, kabla hata ya Instagram haijapamba moto au kuwa na kiki, tulipanga kuwa na mtoto, muda ulipofika tulifanya hivyo japo mwanzoni tulikuwa tunaogopa" amesema T-Bway.
Aidha ameendelea kusema "Kama kuna mwamba aliyevumilia kipindi cha ujauzito basi ni mimi, kuna usiku mmoja alinipigia simu anataka Pizza nikamwambia namtuma mtu au watu wa "Delivery" walete akakataa hadi nikampelekea mwenyewe ila cha ajabu naamka asubuhi hakula hata moja".
"Ilitokea ujauzito wa kwanza tukaenda Hospitali, kuangalia kwenye vipimo haionekani, Daktari akasema tusubiri kama wiki 2, tukirudi nyumbani anaonyesha dalili zote za kuwa mjamzito nikaona ananidanganya hadi tukagombana, nilijua mimi ndiyo tatizo" ameongeza.