Alhamisi , 16th Apr , 2020

Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), imesema kuwa kuanzia kesho Aprili 17, 2020, kila mtu awe mgonjwa, ndugu wa mgonjwa ama mdau yeyote atakayeingia katika taasisi hiyo anatakiwa kuvaa barakoa (Mask).

Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 16, 2020 na Msemaji wa Taasisi hiyo Patrick Mvungi, ambapo amesema kuwa hatua hizo ni kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Hatua hii inakuja ikiwa ni mkakati wa Taasisi kuhakikisha, wagonjwa, ndugu wa wagonjwa pamoja na wadau wetu wanakuwa salama dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona" imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa ni lazima kila mtu kupimwa joto lake la mwili, pamoja na kusafisha mikono kwa kutumia vitakasa mikono kila wanapongia na kutoka.