
Erin Patterson alikuwa na wageni wanne miaka miwili iliyopita wazazi wa mumewe, shangazi yake na mjomba wake, na shangazi wa mumewe
Wageni wanne waliketi kwa chakula cha mchana nyumbani kwake katika maeneo ya mashambani ya Australia mnamo Julai 29, 2023
Ndani ya wiki moja, watatu kati yao walikufa na mmoja akanusurika.
Mwanamke huyo alishtakiwa kwa kuwapa wageni wake sumu kwa kukusudia na uyoga wa porini.
Wakati wa kesi iliyochukua zaidi ya miezi miwili, Bi Patterson alidai kuwa chakula hicho kilitiwa sumu kwa bahati mbaya na uyoga hatari zaidi duniani.
Erin Patterson na mume wake Simon walikuwa wameishi mbali kwa muda mrefu, lakini hawakuachana rasmi.