Alhamisi , 9th Apr , 2020

Leo  Alhamisi Aprili 9,2020, watu wengi ifikapo siku hii kujikumbushia matukio ya zamani yaliyopita kuanzia picha, video na simulizi siku hii huitwa "TBT".

Msanii wa filamu Wema Sepetu

Kupitia ukurasa wa Instagram anaoutumia staa wa filamu hapa nchini Wema Sepetu, amekumbushia tukio lake la kunyoa kipara, huku akieleza kuwa mpenzi wake wa zamani aliipenda style hiyo.

Kwenye post hiyo Wema Sepetu ameandika kuwa  "ThrowBack Thursday, ila kama ni kuthubutu jamani nilijuaga kuthubutu kwa kweli, para kama ngozi halafu nilikuwa naingia popote, muda wowote ninavyotaka hata nikioga nasikia raha, halafu wakati huo aliyekua mpenzi wangu akawa anakihusudu kipara pia, basi mambo yakawa bulbul, maisha haya" ameandika Wema Sepetu.