Ringtone katika maelezo yake haya amesema, Jimmy Gait ni msanii ambaye amekuwa akiimba kwa kutumia staili yake na licha ya hayo amefikia hadi hatua ya kuvaa kama anavyovaa, kitu ambacho kinamsikitisha yeye kama msanii mwenzie.
Kwa sasa bado jitihada zinafanyika kusikia upande wa Jimmy Gait kujua anasema nini juu ya tuhuma hizi, ambazo Ringtone amepigilia msumari kusema kuw anamuombea hasimu wake huyu abadilike na kuendelea bila kuiga kile yeye anachofanya.