Jumatatu , 15th Sep , 2014

Siku kadhaa baada ya msanii Bebe Cool kutoka Uganda kuchaguliwa kuwa balozi wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, Chameleone naye amechukua hatua ya kizalendo na kurekodi wimbo maalum kwaajili ya timu hiyo.

Jose Chameleone (katikati) akiwa na timu yake

Wimbo huu umepatiwa jina Cranes Tubonge na kwa mujibu wa taarifa, utatumika kwaajili ya kampeni maalum kusaidia kuchanga fedha za kuiinua timu hii tayari kwa mashindano ya kombe la Afrika.

Hii imekuwa ni hatua nyingine nzuri ambapo tasnia ya burudani ya muziki na ile ya burudanin ya soka kushirikiana ili kufikishana katika ngazi za juu zaidi.

Bebe Cool na wachezaji wa The Cranes