
Beyonce
Beyonce ameeleza kuwa kwenye filamu yake ya Home coming, Beyonce alikuwa ana kilo 175 baada ya kujifungua watoto mapacha waitwao Rumi Carter na Sir Carter.
Pia tovuti hiyo imeeleza kuwa Beyonce aliandaliwa lishe maalumu ya siku 22 ya kupunguza uzito kutoka kwa rafiki yake, mwalimu wake wa mazoezi na mwanasaikolojia aitwaye Marco Borges, ambaye alikuwa anampatia vyakula vya lishe, mazoezi ya kukimbia na kucheza, kumpa matunda na mbogamboga ndani ya siku 22 tu.
Siku 44 baadaye Beyonce alipungua kutoka kilo 175 hadi kilo 79, na alitumbuiza stejini kwa muda wa masaa mawili kwenye tamasha la Coachella. Katika tamasha hilo Beyonce alilipwa Dola Milioni 4, sawa na Bilioni 9 za Tanzania.