
mtu mwenye msongo wa mawazo
Sio kweli kwamba kila mahusiano huwa yanadumu katika hali ileile, kwani wengine hufikia hatua ya kushindwa kuvumiliana kwa baadhi ya ilhali bado wanapendana. Unaweza ukawa umeachana na mwenza wako kwa ndoa au mahusiano kuvunjika lakini bado ukawa unasumbuliwa na mawazo yake, sasa utawezaje kumsahau?. Mtaalamu wa mahusiano, Godfrey Mshana kupitia DADAZ, ameelezea njia za kufuata ili kumsahau mtu ambaye ulimpenda sana na huwezi kumsahau.
Godfrey amesema kuwa kumbukumbu za mahusiano ni ngumu kusahaulika, lakini inategemea na hisia zenyewe zilikuwa ni za namna gani, mfano ni kwa mtu wa karibu zaidi ama mpenzi wako wa muda mrefu.
"Kwanza kusahau kuko kwa aina mbili, unaweza ukaifuta kabisa kumbukumbu ya mahusiano, lakini unaweza ukawa unashinda kuikumbuka kutokana na vikwazo fulanifulani. Ni kweli kumbukumbu za mahusiano ni ngumu kusahaulika, sasa kama ni ngumu kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifuata ili kusahau", amesema Mshana.
"Njia ya kwanza unatakiwa kujiuliza ni kwanini bado unaendelea kumkumbuka mpenzi wako wa zamani, kwahiyo kwenye majibu yako utajua kweli kama bado unampenda au laa, kama utagundua hamjaachana kweli, basi hatua ya pili tafuta namna ya kuachana, kwa maana wote mkubaliane kuwa sasa mnaachana", ameongeza.
Tazama video hapa chini kutazama njia zingine za kufuata ili kuweza kumsahau mpenzi ambaye bado unamkumbuka.