Alhamisi , 21st Aug , 2014

Wasanii wanaotokea mkoa wa Ruvuma, kwa pamoja wamezindua rasmi kampeni inayojulikana kama 'Bwela Kuni' sambamba na Wimbo wa pamoja uliopatiwa jina 'Bwela Kuni', dhumuni kubwa ikiwa ni kutangaza mkoa huu, vipaji na rasilimali zake kwa watu.

wasanii katika uzinduzi wa kampeni ya 'Bwela Kuni'

'Bwela Kuni', neno la kingoni ambalo lina maanisha njoo hapa, ni kazi ambayo imefanyika chini ya mtayarishaji muziki C9 Kanjenje ambaye ndiye muasisi wa wazo hilo, na hapa anazungumza kwa niaba ya wenzake anaeleza umuhimu wa kazi hii katika kuwainua wasanii wa Ruvuma.

Huu ni mwanzo wa project hii ambayo itahusisha pia wasanii kama vile Professor Jay, Mrisho Mpoto, Mtayarishaji muziki Mr T Touches ambao wote pia ni wanaotoka mkoa wa Ruvuma.