Alhamisi , 14th Aug , 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania waishio nchi za nje kutosahau kurudi nyumbani ili waweze kuitumikia nchi yao kutokana na ujuzi walioupata katika nchi wanazoishi.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Watanzania Waishio Nje ya Nchi leo Jijini Dar es Salaam Dkt. Kikwete amesema umefika wakati kwa watanzania waishio nje ya nchi kuwasaidia watanzania waliopo hapa nchini katika mambo mbalimbali hususan katika sekta ya elimu.

Dkt. Kikwete akizungumzia suala la uraia wa nchi mbili amesema suala hilo watanzania wanaoishi nje ya nchi wanayo nafasi ya kutoa msukumo na kuliundia hoja ili liwepo katika Katiba mpya kutokana na kuwa suala la kikatiba zaidi ni sio suala rahisi na kwa kuwa limetamkwa katika sheria za nchi.

Kwa miaka kadhaa sasa suala la uraia wa nchi mbili limekuwa likijadiliwa bungeni huku wabunge wakitaka itunge sheria ya kutambua uraia wa nchi mbili ili kutoa fursa kwa Watanzania waishio nje ya nchi kushiriki ipasavyo katika ujenzi wa taifa.