
Wakizungumza na East Africa Radio, kwa nyakati tofauti wanawake hao wamesema kuwa kutokuwepo kwa usimamizi wa bei kunasababisha wao kufanya kazi isiokuwa na maslahi.
Kina mama wanaofanya kazi katika eneo hilo wamesema wamejikuta wakilizamika kuuza kokoto hizo kwa bei ya hasara kutokana na kurudishwa nyuma na madalali hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wa kupiga hatua kimaendeleo kupitia shughuli hiyo.
Akizungumzia Suala hilo Mkuu wa Wilaya Tanga, Thobias Mwilapwa, amesema kuwa bei elekezi ya serikali ipo tatizo kina mama hao wanakosa umoja kwa kukubaliana kwa pamoja kufuata bei elekezi na watambue atakenunua chini ya hapo ni kwamba amekiuka sheria.