Jumanne , 1st Jul , 2014

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) Hababuu Ali Omari amefanya mchujo wa wachezaji wanaojiandaa kwa mechi ya mashindano dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Kikosi cha Serenget Boys

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) Hababuu Ali Omari amefanya mchujo wa wachezaji wanaojiandaa kwa mechi ya mashindano dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Kocha Omari amepunguza wachezaji wa timu hiyo kutoka 39 na kubaki na 31 huku Timu hiyo imepiga kambi kwenye hosteli ya Shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF iliyopo Uwanja wa Karume.

Mechi hiyo ya kwanza ya Mzunguko wa pili itachezwa Ijumaa ya Julai 18 mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Akizungumzia maandalizi ya Timu hiyo Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini TFF Bonifasi Wambura amesema kwa sasa timu hiyo ipo katika maandalizi mazuri na wanasubiri tu mpambano huo.