Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake. Hali ya mzee Kingunge inaendelea vizuri kwa sasa.
Jana Mtoto wa Mzee Kingunge, Tony Kingunge aliimbia HOTMIX kwamba sana tofauti na mara ya kwanza alipong'atwa na mbwa baba yao anaendelea na matibabu mengine ya majeraha aliyokua nayo chini ya uangalizi maalum wa madaktari.
Rais Magufuli akisalimiana na Mzee Kingunge katika wodi ya Mwaisela alikolazwa
Mzee Kingunge ambaye amefiwa na mke wake katikati ya wiki hii bado hajapatiwa habari hizo kutokana na hali yake aliyonayo kwa sasa, na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anategemewa kwenda kuongea naye Hospitali na kumfikishia taarifa za msiba huo.
Bi. Peras Kingunge alifariki dunia Alhamisi mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na tatizo la kupooza kwa muda na taratibu za mazishi yake zinasubiri maamuzi ya mumewe, Mzee Kingunge Ngombale ambaye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ambapo kwa sasa msiba upo nyumbani kwake Kijitonyama.