Alhamisi , 30th Jan , 2025

Mahusiano kati ya Rwanda na Afrika Kusini yanaweza kuwa si mazuri kwa sasa hii ni baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kutoa onyo kali kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, akisema kwamba Rwanda imejiandaa kwa lolote iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Taarifa ya Rais Kagame ilikuwa inajibu maoni ya Rais Ramaphosa juu ya jukumu la Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda na Kikundi cha Waasi cha M23 katika mapigano yanayoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jibu la Rais Paul Kagame kwa Cyril Ramaphosa liliashiria mzozo mbaya wa kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Rwanda. Katika taarifa iliyo na maneno makali akimjibu moja kwa moja Cyril Ramaphosa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Kagame alimshtumu Rais wa Afrika Kusini kwa kupotosha mazungumzo ya faragha juu ya hali tete mashariki mwa DRC.

Kiongozi huyo wa Rwanda pia amesema Rais Ramaphosa alikuwa hajaonya Rwanda juu ya shughuli zake za kijeshi DRC lakini badala yake alikuwa ameomba msaada wa vifaa, pamoja na umeme, chakula, na maji kwa wanajeshi wa Afrika Kusini. Wakati akikaribisha juhudi za Afrika Kusini za amani, Bwana Kagame amesisitiza kwamba nchi hiyo haikuwa katika nafasi ya kuwa mtafutaji amani wala mpatanishi na ameonya zaidi kwamba ikiwa Afrika Kusini inataka makabiliano, Rwanda itajibu ipasavyo.