Alhamisi , 30th Jan , 2025

Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki chakula cha mchana na watendaji wa vikosi mbalimbali pamoja na watu walioshiriki katika shughuli ya uokoaji kwenye tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 16, 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Ikulu, Dar es Salaam Rais Samia amesema kuptia tukio hilo Serikali imefahamu namna biashara zinavyoendeshwa katika eneo hilo la Kariakoo.

Amesema taarifa zilizopo zinabainisha kuwa jengo hilo lililoporomoka lilikuwa na uwezo wa kubeba tani 250 za mzigo, lakini wakati linaporomoka lilikuwa na mzigo wa tani 800.

Aidha, Rais Samia amesema somo ambalo Serikali imelipata baada ya kuporomoka kwa jengo hilo la ghorofa la Kariakoo ni kwamba lazima uwepo usimamizi wa kutosha katika ujenzi wa majengo mbalimbali na kuhakikisha vigezo vya ujenzi vinafuatwa.

"kwa wale walioliona jengo unaona kabisa ni mchanga mwingi kuliko saruji, somo jingine ambalo mimi nililoliona kwa haraka haraka na pengine ndilo kwa wakati ule lilileta mzozo kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ni mali inayofichwa mule ndani na bila kulipiwa kodi, sasa jengo lile limetufunulia mambo mengi sidhani kama zile tani 800 mule ndani zililipiwa kodi," amesema Rais Samia