Jumatano , 12th Mei , 2021

Hitmaker wa nyimbo ya mafungu ya nyanya Dayna Nyange ameshea stori yake ya kutaka kuwa na rangi nyeupe hali iliyomfanya kuanza kutumia madawa ya kubadili ngozi ambayo alitumia kwa muda wa mwaka mmoja.

Msanii Dayna Nyange

"Nilipitia situation hiyo ya kutaka kubadili mwili kuwa mweupe kwa sababu mazingira fulani yalitengenezwa kufikia huko na sio kwamba ilikuwa akili yangu kusema nikatafute mafuta ili niwe hivi

"Asilimia ya watoto wa kike hatuwezi kukaa na kitu kimoja, hiyo ilichangia kuelekezwa mafuta ya kwenda kununua na kuanza kupaka, yakaanza kuning'aza kidogo kumbe unatakiwa ukipaka unatulia baada ya wiki mbili, mimi nikatengeneza hadi pipa natumbukia kabisa, nikatoka muarabu mtoto wa Morogoro" amesema Dayna Nyange