Jumatatu , 27th Jan , 2025

Taifa la Colombia limekubali kupokea ndege za kijeshi zilizobeba wahamiaji waliofukuzwa nchini Marekani kwa mujibu wa Taarifa ya ikulu ya nchini Marekani, Taifa hilo la Amerika ya Kusini mara ya kwanza lilikaidi hatua hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuiwekea Colombia ushuru na vikwazo ili kuiadhibu kwa kukataa kupokea ndege za kijeshi zilizowabeba wahamiaji kama sehemu ya sera zake kuondoa uhamiaji nchini humo.

"Serikali ya Colombia imekubali masharti yote ya Rais Trump, ikiwa ni pamoja na kukubali bila ya masharti wageni wote haramu kutoka Colombia waliorejea kutoka Marekani, ikiwa ni pamoja na ndege za kijeshi za Marekani, bila kizuizi au kuchelewa," imesema taarifa hiyo ya ikulu.