
Watoto hao wamepelekwa chini ya ushirikiano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Safari hiyo ya matibabu imejumuisha wauguzi pamoja na wazazi wa watoto ambao kwa pamoja wameondoka nchini Disemba 10 mwaka huu.
Baada ya matibabu ya watoto kukamilika, Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.
Aidha kundi hilo limekuwa ni kundi la tano la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.
Kwa upande mwingine Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imewataka wazazi na walezi kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni.