Jumamosi , 21st Jun , 2014

Staa wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool ameibuka na kuzungumzia bajeti ya nchi hiyo ya mwaka 2014/2015 ambayo imesomwa hivi karibuni, na kuilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kuwawekea wakulima hasa wale wadogo mzigo mzito wa kodi katika pembejeo.

Bebe Cool

Bebe Cool amesema kuwa, wakulima hawa walitakiwa kuzingatiwa na kuondolewa mzigo wa kodi kubwa kutokana na mchango wao mkubwa wa kuipatia nchi hiyo chakula.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Bebe Cool ametoa kile alichokiita ushauri wake kwa Mheshimiwa Rais Museveni kuwa, kuliko kutoza kodi kwa vifaa vya kilimo, ni bora kuongeza kodi zaidi katika vitu vya starehe ili kuepusha njaa katika siku zijazo nchini humo.