Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Akisoma hukumu ya kesi hiyo Jaji kiongozi Fakihi Jundu amesema kesi hiyo imetupiliwa mbali kutokana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walioorodheshwa waliofungua kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kumfungulia kesi Waziri Mkuu.
Jaji Jundu amesema mahakama imesikiliza pande zote mbili na kueleza kuwa kesi hiyo imeonekana ni batili kutokana na Kinga na Haki za Wabunge, Ibara ya 100 (1) na (2) ambapo kwa mujibu wa ibara hiyo, kutakuwa na uhuru wa mawazo na majadiliano bungeni, ambao hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote, au katika mahakama yoyote nchini.
Aidha, wakili kutoka LHRC, Harold Sungusia amesema ameridhishwa na maamuzi ya kesi hiyo na walifungua kesi hiyo kutokana na kupewa mamlaka na Katiba katika ibara 100 kifungu cha pili kinachotoa nafasi kwa mbunge kushitakiwa mahakamani kutokana na kauli zake ndani ya bunge