Jumapili , 1st Jun , 2014

Ikulu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imekana kuwa na taarifa za madai ya uchochezi unaofanywa na balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose, kama zilivyotolewa na wizara ya nishati na madini.

Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue. Ofisi yake imekana kuwa na taarifa ya tuhuma za kuingilia mambo ya ndani zinazomkabili balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose.

Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue, amesema taarifa hizo hajiwahi kuwepo mezani kwa Rais Kikwete wala kwenye ofisi yoyote ya Ikulu na kwamba yeye hazifahamu.

Tuhuma dhidi ya balozi Melrose zimetolewa bungeni mjini Dodoma juzi, na naibu waziri wa nishati na madini Steven Maselle, wakati akichangia majumuisho ya hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, ambapo amemtuhumu balozi huyo kwa kushawishi nchi wahisani zisiisaidie Tanzania, na kumtaka balozi huyo kufika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kujieleza.