Jumatatu , 19th Mei , 2014

Zaidi ya kaya 250,000 zitaanza kunufaka na mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Tanzania unaolenga kuboresha maisha ya wafugaji wadogo katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe.

Zaidi ya kaya 250,000 zitaanza kunufaka na mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Tanzania unaotekelezwa na shirika la Heifer International kwa kushirikiana na mashirika mengine unaolenga kuboresha maisha ya wafugaji wadogo, ambapo katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe zaidi ya familia 35,000 zitafikiwa moja kwa moja na mradi huo.

Meneja wa mradi huo nchini Tanzania Bwana Mark Tsoxo akizungumza mkaoni Mbeya  amesema zaidi ya dola Mil. 12 zitatumika kwa kipindi cha miaka mitano cha awamu ya pili ili kufanikisha uendelevu wa kujikimu katika kaya za kifugaji, anasema kwa Afirika Mashariki, Uganda na kenya ni miongoni mwa nchi unako tekelezwa mradi huo:.

Katibu tawala wa mkoa wa mbeya bi. Mariam mtunguja amesema pamoja na kanda ya nyanda za juu kusini kuwa na uzalishaji mkubwa wa maziwa, lakini kuna malisho duni, miundombinu hafifu, ukosefu wa mfumo rasmi wa soko la maziwa hata kiwango kidogo cha unywaji maziwa kinaumiza wafugaji na kusababisha tija ndogo ikilinganishwa na fursa zilizopo:..

Tanzania inakadiriwa kuwa na ng'ombe wa maziwa zaidi ya Mil. 22 lakini ni asilimia 3 ya ng'ombe mahususi wanaozailisha maziwa, pengine kupitia mradi huu unaodhaminiwa na mfuko wa Bill na Melinda unaweza kuongeza kiwango cha uzalishaji kutoka lita za maziwa saba zinazo zalishwa kwa sasa hadi kufikia lita 18 mpaka 20 hapo badaye.