Dully Sykes
Dully amefunguka hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, ambapo amesema hana haja ya yeye kujiunga na lebo nyingine yoyote ya muziki kwa kuwa na yeye ana mpango huo.
Amesema lebo hiyo itakuwa kamili mapema mwakani na kwamba tayari amekwishaanza kukusanya vipaji vipya, huku akisisitiza kuwa katika lebo yake hakutakuwa na mastaa, anataka awe na wasanii wachanga ambao anawazidi na amewatangulia.
"Na mimi naanzisha lebo yangu kuanzia Januari, sina haja ya kwenda kwa Diamond, nishaanza maandalizi, nina studio nina wasanii, lakini sitataka wasanii wanaonizidi, nitataka wasanii wachanga zaidi" Amesema Dully Sykes
Amesema kikwazo kikubwa cha wasanii wa Bongo ni menejimenti kwahiyo anachotamani kufanya ni kutengeza menejimenti imara kama ilivyo kwa menejimenti za Diamond na Alikiba.
Katika hatua nyingine, Dully ametoa taarifa rasmi kuwa anatoa ngoma mpya kabla ya mwezi Februari mwaka 2017 ambayo itakuwa ni hatari kuliko Inde.