Ijumaa , 16th Mei , 2014

Rapa Octopizzo ameamua kuleta ladha ya tofauti katika sanaa ya video za muziki Afrika Mashariki, ambapo yupo katika mchakato wa kutengeneza video inayohusisha matukio yaliyoongezewa vionjo na teknolojia ya sayansi ya kubuni, (Science Fiction).

Octopizzo

Video hii inatarajiwa kuwa kivutio cha aina yake pindi itakapotoka na pia itakuwa ni production ya kwanza ya aina hii kwa msanii kutoka Afrika Mashariki Kufanya, ikiwa ni mchakato wa msanii huyu kutaka kuleta tofauti katika sanaa.

Video hii ni ujio mwingine mkubwa kabisa wa Octopizzo ingawa mpaka sasa bado kiasi cha pesa ambacho msanii huyu amewekeza katika kufanya kazi hii hakijafahamika, na wala jina la kazi yenyewe.

Tags: