
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameliambia Bunge la Tanzania kuwa Ushawishi wa Tanzania katika medani za Kimataifa umeongezeka chini ya Serikali ya awamu ya sita na kuiwezesha Tanzania kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika mashirika ya Kikanda.
Majaliwa amebainisha hayo wakati wa Hotuba yake ya kuhitimisha mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Tanzania leo Juni 26, 2025, akimtaja kwa mfano Dkt. Ntuli Kapologwe aliyechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini pamoja na Prof. Mohamed Janabi, aliyechaguliwa kywa Mkurugenzi wa Shirika la Afya duniani, Kanda ya Afrika.
"Nitumie fursa hii kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hasdan kwa kuimarisha uhusiano huu wa Kimataifa na diplomasia ya uchumi. Maono yake katika kufikia azma ya kuinganisha Tanzania na Mataifa mengine kiuchumi na kisiasa yamewezesha kupata mafanikio makubwa." Amesema Mhe. Majaliwa.
Aidha Majaliwa amebainisha mafanikio mengine kuwa ni pamoja na Rais Samia kupokea uenyekiti wa Asasi za siasa, ulinzi na usalama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC, ambapo chini ya uenyekiti wake pamoja na masuala mengine, Tanzania imeweza kusimamia uangalizi wa Chaguzi kwenye nchi za Botswana Mauritius. Msumbiji na Namibia.
Aidha Tanzania pia imefanikiwa kuratibu ziara za kimkakati za Viongozi 2a Kitaifa nje ya nchi, pamoja na kupokea Viongozi wa Kimataifa waliotembelea Tanzania, ziara ambazo zimefanikisha kufikiwa kwa makubaliano na kusainiwa kwa mikataba ya ushirikiano kwaajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo katika sekta za kipaumbele.
"Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba kati ya China, Zambia na Tanzania kwa lengo la kufufua reli ya TAZARA ili kuboresha huduma za reli hiyo." Ameongeza Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha mafanikio mengine yaliyofikiwa ni pamoja na kushiriki kikamilifu mikutank, makongamano na majukwaa mbalimbali yanayolenga kuimarisha ushirikiabk wa Kimataifa katika kukabiliana na changamoto za kidunia ikiwa ni pamoja na ushiriki wa Mkutank wa wakuu wa nchi Tajiri dunianu za kundi la G20 na Mkutank wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya tabianchi.