
Makamu wa Rais katika shule za sekondari Idetemya
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika ziara yake inayoendelea mkoani Mwanza ambapo akiwa katika wilaya za Kwimba na Misungwi leo amezindua mabweni ya wanafunzi wa kike katika shule za sekondari Idetemya na Askofu Mayalla.
Akiweka jiwe la msingi katika mojawapo ya mabweni ya wasichana katika shule ya Askofu Mayalla, Makamu wa Rais ameahidi kuchangia mifuko 200 ya saruji pamoja na mabati 100 ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazooneshwa na shule hiyo za kuwaokoa watoto wa kike.
Awali katika uzinduzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Idetemya wilayani Misungwi, Mhe. Samia amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kusomea watoto wa kike kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kujenga mabweni mengi zaidi.
Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule ya Askofu Mayalla inayohudumia wasichana ambao walikumbwa an matatizo ya mimba za utotoni na kukosa karo, Katibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza, Moses Mapera, amesema bado kuna upungufu wa vyumba vya madarasa, mabweni na maktaba....